Connect with us

DRC:Kipa mwenye “madoido” Robert Kidiaba kuwania ubunge

DRC:Kipa mwenye “madoido” Robert Kidiaba kuwania ubunge

Na Victor Abuso,

Wachezaji wawili wa klabu ya soka ya TP Mazembe nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  wakiongozwa na mlinda mlango Robert Muteba Kidiaba, wamewasilisha maombi ya kuwania ubunge katika jimbo la Katanga.

Pamoja na Kidiaba ambaye  anafahamika sana kwa mtindo wa kusherehekea bao kwa kuruka kwa makalio.

Pamphile Mihayo Kazembe pia ni mchezaji mwingine wa TP Mazembe anayewania ubunge kupitia chama cha upinzani cha  PND. 

Nahodha huyo wa Leopards mwenye umri wa miaka 39 amesema anaamini kuwa wachezaji wanaweza kuwa viongozi bora na kuleta mabadiliko ya maendeleo katika maeneo yao.

Uchaguzi wa wabunge na urais utafanyika mwaka ujao nchini humo na ikiwa Kidiaba atachaguliwa kuwa mbunge, bila shaka itakuwa ni historia katika mchezo wa soka nchini humo.

Kidiaba alianza kuichezea timu ya taifa mwaka 2002 na ameshiriki katika michuano 11 ya kufuzu katika michuano ya kombe la duniani na kwa ujumla kuichezea timu ya taifa mara 59.

Mwezi Desemba, mwaka 2014 alitangaza kuwa alikuwa anajiuzulu baada ya michuano ya mwaka huu ya mataifa bingwa barani Afrika lakini baadaye akabadilisha mawazo ya kuendelea kucheza soka.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in