Connect with us

Swahili Stories

Droo ya fainali yavijana kutolewa Alhamisi

Droo ya fainali yavijana kutolewa Alhamisi

Na Victor Abuso,

Droo ya michuano ya bara Afrika, kuwania taji la vijana wasiozidi miaka 17 itafanyika siku ya Alhamisi jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Michuano hiyo ya 13, itafanyika jijini Dar es salaam nchini Tanzania kati ya tarehe 14 hadi 28 mwezi Aprili mwaka 2019.

Wenyeji Tanzania, ni miongoni mwa mataifa nane, yaliyofuzu kucheza katika fainali hiyo.

Mataifa mengine yatakayopambana kutafuta ubingwa huo ni pamoja na Morocco, Senegal, Guinea, Nigeria, Cameroon, Uganda na Angola.

Mataifa yatakayofika katika hatua ya nusu fainali, yatafuzu kushiriki katika kombe la dunia mwaka 2019 nchini Peru.

Mabingwa watetezi Mali, walishindwa kufuzu katika fainali ya mwaka 2019.

More in Swahili Stories