Connect with us

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Gor Mahia nchini Kenya Dylan Kerr, ameajiriwa na klabu ya Afrika Kusini Black Leopards.

Raia huyo wa Uingereza, aliyeujizulu kutoka Gor Mahia wiki iliyopita, anachukua nafasi ya Joel Masutha aliyeachia nafasi hiyo wiki iliyopita kwa sababu ya matokeo mabaya.

Anachukua uongozi wa klabu ambayo inashikilia nafasi ya 14 kati ya klabu 16 zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini, na kazi kubwa ni kuisaidia kupanda hadi katika nafasi za juu, katika msururu wa ligi kuu.

More in East Africa