Connect with us

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, inayowajumuisha wachezaji wenye chini ya umri wa miaka 23, walianza vema kampeni ya kufuzu katika fainali ya bara Afrika mwaka 2019 nchini Misri, baada ya kuifunga Mauritus mabao 5-0.

Emerging Stars, ilipata ushindi huo mkubwa katika mechi iliyochezwa siku ya Jumatano jioni latika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.

Mabao ya Johnston Omurwa, James Mazembe, Piston Mutamba, Sidney Lokale na Joseph Okumu yanaiweka Kenya katika nafais nzuri ya kufuzu katika hatua ya pili ya michuano hiyo, itakaporudiana na Mauritius tarehe 18 mwezi huu.

Matokeo zaidi:-

Burundi2-0 Tanzania

Ethiopia 4-0 Somalia

Rwanda 0-0 DRC

Uganda 1-0 Sudan Kusini

Ushelisheli 1-1 Sudan

Mataifa nane yatafuzu kushiriki katika fainali hiyo. Nigeria ndio mabingwa watetezi.

Mashindano ya bara Afrika kufanyika kila baada ya miaka minne.

Timu tatu bora, zitafuzu katika fainali ya michezo ya Olimpiki nchini Japan mwaka 2020.

Afrika Kusini,Zimbabwe, Zambia, Congo Brazzaville, Gabon, Algeria, Sierra Leone, Tunisia, Ivory Coast, Senegal, Nigeria, Morocco na Mali zimefuzu katika hatua ya pili ya michuano hii.

More in East Africa