Connect with us

Mabingwa watetezi wa taji la bara Afrika katika mchezo wa soka, Super Falcons ya Nigeria, hatimaye wamefufua matumaini ya kusonga mbele katika fainali zinazoendelea jijini Accra nchini Ghana, kutafuta ubingwa wa Afrika,  baada ya kuifunga Zambia mabao 4-0 katika mechi yake ya pili Jumatano usiku.

Huu ni ushindi muhimu kwa Nigeria, ambao walianza vibaya michuano hii baada ya kufungwa na Afrika Kusini bao 1-0.

Hata hivyo, mambo yanaendelea kuwa mabaya kwa Equitorial Guinea ambao walipoteza mechi yake ya pili baada ya Afrika Kusini kupata karamu ya mabao 7-1.

Baada ya matokeo hayo, Afrika Kusini inaongoza kundi la B, kwa alama 6, huku Nigeria na Zambia zikiwa na alama tatu.

Kesho kutakuwa na michuano za kumaliza kundi A, Cameroon watachuana na Ghana, huku Algeria wakicheza na Mali.

More in AWCON