Connect with us

 

Ethiopia na Tanzania zimeungana na Kenya katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la mchezo wa soka la CECAFA kwa upande wa wanawake.

Timu ya taifa ya Ethiopia inayofahamika kama Lucy, ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuifunga Rwanda mabao 3-2 katika mchuano muhimu katika taasisi ya Njeru mjini Jinja nchini Uganda Jumatano jioni.

Wachezaji wa Ethiopia, walionesha kiwango cha kuvutia uwanjani wakicheza pasi fupifupi na kuwafurahisha mami ya mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mchuano huo.

Mabao ya Ethiopia yalifungwa na Sisaya Shetaye, Girma Berktawit na Losa Abera.

Michuano ya hatua ya makundi inamalizika siku ya Alhamisi kwa Kenya kumenyana na Zanzibar, huku mchuano mwingine muhimu wa kuamua ni nani atafuzu katika hatua ya nusu fainali ikiwa ni kati ya wenyeji Uganda na Burundi.

More in East Africa