Connect with us

Baraza la mchezo wa soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA, limeifungia Zanzibar na Ethiopa na kuzitoa faini baada ya kubainika kuwa na vijana wenye umri mkubwa katika mashindano ya vijana wasiozidi miaka 17 yanayoendelea nchini Burundi.

Baada ya uchunguzi,  CECAFA imebaini kuwa Zanzibar ilikuwa na wachezaji tisa waliokuwa na umri mkubwa huku Ethiopia ikiwa na wachezaji watatu.

Kabla ya mashindano haya, CECAFA ilikuwa imetoa mwelekeo kuwa, wachezaji wanaostahili kushiriki katika michuano hii ni wale waliozaliwa baada ya mwaka 2002 na sio kabla ya mwaka huo.

Zanzibar, ambayo imeondolewa katika mashindano hayo, haitashiriki katika michuano ya CECAFA hadi ikapolipa fainali ya  Dola 15,000.

Ethiopia pia imetakiwa kulipa faini ya Dola 5,000.

More in African Football