Connect with us

Shirikisho la soka nchini Rwnada FERWAFA limelazimika kuchelewesha kuanza kwa michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA kwa upande wa wanawake, yaliyokuwa yameratibiwa kuanza tarehe 12 mwezi Mei.

FERWAFA inasema imechukua hatua hiyo kwa sababu bado inasubiri msaada wa kifedha kutoka kwa uongozi wa CECAFA.

Msemaji wa FERWAFA Bonnie Mugabe amesema  Rwanda ilikuwa tayari kuandaa michuano hiyo lakini haijasikia lolote kutoka kwa CECAFA licha ya kujaribu kuwasiliana na uongozi wa Baraza hilo.

Haijafahjamika sasa ni lini michuano hii itafanyika.

FIFA ilikuwa imetoa kiasi fulani cha fedha kufanikisha michuano hii, lakini haijafahamika iwapo fedha hizo zimefikia CECAFA kupitia Shirikisho la soka barani Afrika CAF.

More in African Football