Connect with us

FIFA: Uganda yaendelea kuongoza ukanda wa CECAFA

FIFA: Uganda yaendelea kuongoza ukanda wa CECAFA

 

Shirikisho la soka duniani FIFA, limetangaza orodha ya mataifa bora duniani mwezi huu wa tano.

Duniani, Argetina ni ya kwanza, ikifuatwa na Ubelgiji. Nafasi ya tatu imeiendea Chile, nafasi ya nne Colombia huku Ujerumani ikifunga tano bora.

Barani Afrika, Algeria ni ya kwanza lakini ya 33 duniani. Cote Dvoire ni ya pili huku ikiwa ya 34 duniani, huku Ghana ikishika nafasi ya tatu barani Afrika lakini ni ya 38 duniani.

Senegal ni ya nne, Misri ya tano, Cape Verde ya sita barani Afrika na ya 47 duniani huku Tunisia ikiwa ya saba wakati DRC ikifunga nane bora barani Afrika lakini inashikilia nafasi ya 51 duniani.

Uganda inaendelea kuongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, na ni ya 16 barani Afrika na ya 72 duniani.

Rwanda ni ya pili, 21 barani Afrika na 87 duniani. Kenya ni ya tatu, inashikilia nafasi 33 barani Afrika na ya 116 duniani. Burundi ni ya 37 barani Afrika na ya 123 duniani. Tanzania nayo ni ya 41 barani Afrika huku ikiwa ya 129 duniani.

Djibouti, Eritrea na Somalia zinashikilia nafasi ya mwisho katika orodha ya mwezi huu.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in