Connect with us

Ghana: Asamoah Gyan astaafu soka

Nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Ghana Asamoah Gyan, ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya soka, wiki chache kuelekea fainali ya kuwania taji la Afrika nchini Misri.

Gyan amesema amefanya uamuzi huo baada ya kocha Kwesi Appiah kutomteua kuwa nahodha wa timu ya taifa wakati wa mashindano hayo makubwa barani Afrika yatakayofanyika mwezi Juni.

“Baada ya mashauriano na familia yangu na timu, iwapo uamuzi wa kocha ni kumpa unahodha mchezaji mwingine na ameniita katika kikosi chake, basi naomba nijiondoe,” amesema Gyan mwenye umri wa miaka 33.

Mchezaji hiyo anayechezea klabu ya Kayserispor nchini Uturuki, amesema amechana kabisa na timu ya taiga.

“Nastaafu kuichezea timu ya taifa, “ aliongeza.

Gyan alianza kuichezea timu ya taifa mwaka 2003 wakati akiwa na miaka 17 na katika mechi 106 alizoichezea, amefuga mabao 51.

Amewahi kuichezea Ghana katika kombe la dunia mwaka 2006, 2010 na 2014.

Kuelekea katika fainali ya AFCON, Ghana imepangwa katika kundi moja la F na Cameroon, Benin na Guinea-Bissau.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in