Connect with us

Mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia, wanamenyana na Lydia Ludic ya Burundi, katika mchuano wake wa pili kuwania taji la CECAFA, baina ya vlabu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Michuano hiyo imeingia wiki ya pili jijini Dar es salaam nchini Tanzania, katika uwanja wa Chamazi na ule wa Taifa.

Gor Mahia ilianza michuano hii kwa kupata sare ya mabao 2-2 na Rayon Sport ya Rwanda mwishono mwa wiki iliyopita.

Rayon Sport ya Rwanda nayo inamenyana na AS Ports ya Djibouti katika mchuano wake wa pili.

Kundi B, kuna Rayon Sport, Gor Mahia, Lydia Ludic na AS Ports.

Siku ya Jumatatu katika mechi za kundi C, Simba walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya APR ya Rwanda huku Singida ya Tanzania ikipata ushindi wa bao 1-0.

Ratiba ya Jumatano, Julai 4 2018

Vipers (Uganda) vs Kator FC (Sudan Kusini)

APR (Rwanda) vs Dakadaha (Somali)

Simba (Tanzania) vs Singida (Tanzania)

Azam (Tanzania) vs JKU (Zanzibar)

Alhamisi Julai 7, 2018

AS Ports (Djibouti) vs Gor Mahia (Kenya)

Lydia Ludic (Burundi) vs Rayon Sports (Rwanda)

More in African Football