Connect with us

Klabu ya Gor Mahia itakabidhiwa rasmi ubingwa wa ligi kuu nchini Kenya tarehe 18 mwezi Novemba mjini Kisumu.

Hili limethibitishwa na rais wa klabu hiyo Ambrose Rachier.

Gor Mahia ilishinda ubingwa wa ligi kuu nchini Kenya kwa mara ya 16, mechi nne kabla ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu.

K’Ogalo itamenyana na Sony Sugar katika mchuano wake wa mwisho, siku ambayo watakabidhiwa kombe hilo.

Uongozi wa Gor Mahia ulikosa kupata nafasi ya klabu hiyo kucheza mechi hiyo katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani na hivyo kulazimika kwenda mjini Kisumu, Magharibi mwa nchi hiyo.

Gor Mahia itawakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka ujao.

Mwaka 1987, Gor Mahia ilinyakua taji la Afrika, matokeo ambayo hayajaonekana katika siku za hivi karibuni.

More in East Africa