Connect with us

Klabu ya Gor Mahia ya Kenya itamenyana na Simba FC ya Tanzania katika fainali ya kuwania taji la SportPesa, siku ya Jumapili.

Gor Mahia ambayo ni mabingwa watetezi, ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuishinda Singida United ya Tanzania mabao 2-0.

Mabao ya Gor Mahia yalitiwa kimyani na mshambuliaji Meddie Kagere, katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Mchuano mwingine wa nusu fainali,  Simba FC iliishinda Kakamega HomeBoys mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti, baada ya mchuano huo kumalizika kwa kutofungana.

Mshindi kati ya Gor Mahia na Simba FC, itamenyana na klabu ya Uingereza Everton katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki katika uwanja wa Goodison Park mwezi ujao, lakini pia atapata kombe la Dola elfu 30,000.

More in African Football