Connect with us

Gor na AFC zaondolewa taji la SportPesa

Mabingwa watetezi wa taji la SportPesa, Gor Mahia ya Kenya, wameondolewa katika michuano hiyo, baada ya kufungwa na Mbao FC ya Tanzania kwa mabao 4-3 katika mechi ya mwondoano, kupitia mikwaju ya penalti.

Mchuano huo uliopigwa Jumatano mchana katika uwanja, wa Taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania, ulifika katika hatua hiyo baada ya kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Matumaini ya Gor Mahia kusonga mbele yalivunjika baada ya penalti ya nahodha Harun Shakava kuokolewa na kipa wa Mbao FC Metacha Mnata.

Wachezaji wa Gor Mahia waliofunga mabao ni pamoja na Francis Kahata, Jacques Tuyisenge na Boniface Omondi huku Said Hamis, Ngalema, Ibrahim Hashimu na David Mwasa wakiifungia Mbao FC.

Mbali na Gor Mahia, wawakilishi wengine wa Kenya AFC Leoaprds, nao wameondolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa na mabingwa wa soka nchini Tanzania Simba FC bao mabao 2-1.

Kuelekea katika michuano ya nusu fainali, klabu za Tanzania zilizofuzu ni pamoja ni Mbao, Simba huku Kenya ikiwa ikiwalishwa na Bandari na Kariobangi Sharks.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in