Connect with us

Guinea yailemea Tanzania michuano ya vijana nchini Uturuki

Serengeti Boys

Timu ya taifa ya soka ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys, walio na chini ya miaka 17, walianza vibaya michuano ya UEFA Assist U-17 baada ya kufungwa na Guinea 1-0 nchini Uturuki hapo jana.


Tanzania imepangwa Kundi A pamoja na Guinea, Australia na wenyeji, Uturuki, huku kundi la B, likiundwa na Cameroon, Uganda, Morocco na Belarus.

Kundi la C lina, Senegal, Nigeria, Angola na Montenegro.


Tanzania inatumia michuano hiyo kujiandaa kwa fainali ya vijana barani Afrika chini ya miaka 17, itakayofanyika kati ya tarehe 14 hadi 28 mwezi Aprili, itakayofanyika jijini Dar es salaam.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in