Connect with us

Harambee Starlets yalazimisha sare dhidi ya Twiga Stars ugenini

Harambee Starlets yalazimisha sare dhidi ya Twiga Stars ugenini

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars, ililazimisha sare ya bao 1 kwa 1 na Harambee Starlets ya Kenya katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita visiwani Zanzibar.

Starlets ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika kipindi cha kwanza kupitia Tabatha Chacha na baadaye Twiga Stars kusawazisha katika kipindi cha pili kwa kufunga penalti iliyotiwa kimyani na Asha Rashid.

Mchuano huu ulikuwa muhimu kwa Twiga Stars ambao wamepiga kambi Zanzibar kujiandaa kwa michuano ya Afrika itakayoanza mwezi ujao jijini Brazaville nchini Congo.

Kenya walishindwa kufuzu lakini walitumia mchuano huo kuendelea kujiweka katika hali nzuri kwa mashindano yajayo.

Tanzania ambayo itakuwa inashiriki katika mashindano haya kwa mara ya kwanza, itajumuika na wenyeji wao Congo Brazaville, Ivory Coast, Nigeria ambao wamecheza mara 2, sawa na Cameroon.

Mataifa mengine ni pamoja na Afrika Kusini, Misri na Ghana.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in