Connect with us

Harambee Stars yaanza mazoezi dhidi ya Guinea Bissau

Harambee Stars yaanza mazoezi dhidi ya Guinea Bissau

Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars , imeanza mazoezi katika uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi, kujiandaa dhidi ya Guinea Bissau katika mchuano muhimu wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Gabon.

Mazoezi hayo yanaongozwa na kocha mpya wa Stars Stanley Okumbi ambaye alipewa kibarua hicho na rais mpya wa shirikisho la soka nchini humo Nick Mwendwa.

Kenya ina wiki moja kujiandaa kwa mchuano huo utakaochezwa mjini Bissau siku ya Jumatano juma lijalo, kabla ya mchuano wa marudiano tarehe 27 jijini Nairobi katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Kocha Okumbi amesema, ana matumaini makubwa kuwa vijana wake watafanya vizuri katika mchuano huo pamoja na kwamba haifahamu vema Guinea Bissau.

Huu ndio utakuwa mchuano wa kwanza kwa kocha huyu wa nyumbani aliyechukua nafasi ya Bobby Williamson.

Kenya iko katika kundi la E na ni ya tatu kwa alama 1. Congo Brazaville ni ya kwanza kwa alama 4, Zambia ni ya pili pia kwa alama 4 huku Guinea Bissau ikiwa ya mwisho kwa alama 1.

Ligi kuu ya Kenya imesitishwa hadi tarehe 30 mwezi huu ili kuipitisha timu ya taifa kufanya mazoezi.

Kikosi kilichoitwa na kocha Okumbi ni:-

Makipa- Arnold Origi (Lillestrom, Norway), Boniface Oluoch (Gor Mahia), Lucas Indeche (AFC Leopards), Ian Otieno (Posta Rangers);

Mabeki – Harun Shakava, Musa Mohammed (Gor Mahia), Brian Birgen, Omar Mbongi (Ulinzi Stars), Shariff Mohammed (Bandari), David Owino (Zesco United), James Situma (Tusker), Eugene Ochieng (Sony Sugar), Joseph Okumu (Chemelil Sugar) and Brian Mandela (Maritzburg United, South Africa);

Viungo wa Kati – Victor Wanyama (Southampton, England), Johannah Omollo (Antwerp, Belgium), Collins Okoth, Francis Kahata (Gor Mahia), Patillah Omotto (Kariobangi Sharks), Johannah Erick, Roy Syamba (Mathare United), Clifton Miheso, Simon Abuko (AFC Leopards), Anthony Kimani, Shaban Kenga, David Kingatua (Bandari) Ayub Timbe (Lierse, Belgium) ), Anthony Akumu (Zesco United, Zambia), Paul Were (Kalloni, Greece);

Washambuliaji- Michael Olunga (IF Djugardens, Sweden), Aziz Okaka (Ushuru), Timothy Otieno (Posta Rangers), Jesse Were (Zesco United, Zambia), Ovella Ochieng (Kariobangi Sharks) and Nicholas Kipkurui (Zoo Kericho)

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in