African Football

Harambee Stars yapata ushindi mwingine mchuano wa Kimataifa wa kirafiki

on

 

Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, ilipata ushindi mwingine katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kwa kuifunga Liberia bao 1-0 katika mchezo uliopigwa siku ya Jumanne jioni katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.

Ushindi huu unakuja baada ya kupata ushindi mwingine mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuifunga Msumbiji bao 1-0.

Mshambuliaji Paul Were ndiye aliyeifungia timu yake bao la ushindi katika mchuano huo muhimu.

Ushindi huu wa Harambee Stars unaendelea kumpa heshima kocha Okumbi ambaye kwa mechi tisa za Kimataifa akiwa mkufunzi wa kikosi hicho cha Taifa, hajafungwa hata mchuano mmoja.

Kipa wa Liberia Tony Songo alikuwa na wakati mgumu katika lango lake akitumia muda mwingi kuokoa mashuti mazito kutoka kwa washambuliaji kama Michael Olunga na Eric Johanna.

Wachezaji wengine wa Kenya waliotawala mchuano huo ni pamoja na nahodha Victor Wanyama, Abud Omar na Jockins Atudo aliiyeingia kuchukua nafasi ya Teddy Akumu.

Huu ulikuwa ni mchuano wa tatu kwa mataifa haya mawili kukutana baada ya kukutana mara ya mwisho mwaka 1989 wakati wa mchuano wa kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Italia.

 

 

About Victor Abuso

You must be logged in to post a comment Login