Connect with us

Hat-trick dhidi ya Yanga yampeleka timu ya taifa nchimbi

Hat-trick dhidi ya Yanga yampeleka timu ya taifa nchimbi

Sare ya 3-3 ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Yanga SC iliyochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, imempa nafasi timu ya Taifa Ditram Nchimbi.

Kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars Etienne Ndairagije ameamua kumuongeza Nchimbi katika kikosi cha Taifa Stars ikiwa ni siku moja imepita toka mchezaji huyo afunge hart trick dhidi ya Yanga katika sare ya 3-3.

Nchimbi alifunga magoli hayo dakika ya 34, 55 na 58 huku Yanga wakifanikiwa kupata magoli yao ya kupitia kwa Mrisho Khalfan Ngassa dakika ya 16 na David Molinga aliyefunga magoli mawili dakika 65 na 68.

Hivyo ni wazi sasa Nchimbi atakuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 29 wa Taifa Stars watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kalenda ya FIFA kati ya Tanzania dhidi ya Rwanda utakaochezwa Oktoba 14 2019 Kigali, Rwanda.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in