Connect with us

Kocha wa timu ya Taifa ya Misri, Muargentina Hector Cuper amesema uamuzi wa kumuacha nje Mohammed Salah alilenga kumuepusha na hatari zaidi mchezaji huyo.

Salah alikuwa benchi wakati timu ya taifa ya Misri ilipochuana na Uruguay na kushuhudia Misri ikipoteza pambano la ufunguzi kwa bao 1-0 lililofungwa dakika za mwisho na Jose Jiminez.

“Mohammed Salah ni mchezaji mzuri kwenye kikosi chetu, lakini unatakiwa kuwa na timu nzuri na tuna timu nzuri,:amesema Kocha huyo baada ya mchezo.

Cuper aliongeza kuwa Salah atakuwemo kwenye kikosi cha Misri kitakachocheza mechi zinazofuata. Misri itachuana na wenyeji Urusi na Saudi Arabia katika Kundi A.

Misri bado ina rekodi ya kutoshinda michezo mitano iliyopita ya Kombe la dunia. Ietoka sare mechi mbili na kufungwa micheszo mitatu.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in