Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Pilika pilika za kuelekea mchezo wa Simba na Yanga zimeanza jijini Dar es Salaam.

Timu hizo zitavaana Kwenye mchuano wa Ligi Kuu utakaopigwa Oktoba 28 katika Uwanja wa Uhuru.

Yanga imemaliza wikendi kwa kuizamisha Stand United Mabao 4-0 na kuijibu Simba ambayo Jana iliichakaza Njombe Mji idadi kama hiyoo.

Taarifa kutoka mjini Dar es Salaam ni kwamba Simba inatarajia kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo huo.

“Timu inaondoka Jumatano, na tutakuwa huko hadi siku moja kabla ya mchezo,”amesema Ofisa Habari wa Simba Haji Manara.

Bado haijafahamika Yanga itaweka kambi wapi lakini duru za taarifa zinasema huenda ikaweka kambo Mkoani Morogoro.

Gumzo la mchezo huo limeanza kutawala ambapo mashabiki wameanza kutambia katika vijiwe mbalimbali vya jiji.

More in