Connect with us

Klabu ya soka ya Uingereza ya Hull City imeifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti katika  wa mchuano wa Kimataifa wa kirafiki jijini Nairobi.

Mchuano huo ulikwenda katika hatua penalti, baada ya kumaliza kwa kutofungana, katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya mashabiki katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani.

Kampuni ya michezo nchini Kenya ya kubahatisha SportPesa inayofadhili klabu zote mbili, ndiyo iliyopanga mchuano huo wa kirafiki.

Ulikuwa ni mchuano wa saba wa kirafiki kati ya Gor Mahia na timu za Uingereza katika historia yake ya soka.

Mwaka 1983, Gor Mahia iliwahi kucheza na Norwich City na kuishinda mabao 4-2.

Mwaka 1984, Gor Mahia pia ilicheza na Notts County na kufungwa mabao 3-2 lakini mwaka uliopita wa 2017, ilicheza na Everton na kufungwa mabao 2-1.

 

More in East Africa