Connect with us
Na Clarisee Uwimana,
Kabla ya kucheza na Tunisia, tutapiga kambi nchini Morroco tarehe 26 bila ya wachezaji wawili muhimu.
Kocha Florient Ibenge wiki hii, alikitaja kikosi cha wachezaji  28, bila ya wachezaji Yusuf Mulumba na Dieumerci Mbokani, anayechezea Dinamo Kiev.
Kikosi hicho kinajiandaa katika mechi muhimu ya kufuzu kombe la dunia  Urusi mwaka 2018.
Timu zote zina alama sita baada ya mecho sita na kocha Ibenge amesema wataenda Tunis kutafuta alama tatu muhimu.
“Tutaenda huko kutafuta alama tatu, tukipata moja sio mbaya,” alisema Ibenge.
Kufikia tarehe 27, wachezaji wote wanatarajiwa kuwa nchini Morroco watakakotokea moja kwa moja kwenda Tunisia.

More in