Connect with us

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya DRC,  Florent Ibenge amesisitiza kuwa hana mipango yoyote ya kumwita beki Chris Mavinga katika kikosi cha timu ya taifa.

Ibenge ametoa kauli hii baada ya mchezaji huyo anayecheza soka kulipwa  katika klabu ya Toronto FC kumtaka kocha huyo kumfafanulia ni kwanini hakumwita katika kikosi cha wachezaji 26, kinachojiandaa kumenyana na Tanzania katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki jijini Dar es salaam baadaye mwezi huu.

Kocha Ibenge wiki hii aliimbia RFI Kifaransa kuwa aliamua kuendelea kumtazama mchezaji huyo na kumhimiza aendelee kutia bidii katka klabu yake.

Hata hivyo, Mavinga mwenye umri wa miaka 26, ambaye amewahi kuichezea Leopard mara mbili mwaka 2015, kupitia ukurasa wake wa Twitter hakuridhishwa na uamuzi wa kocha huyo.

 

More in African Football