Connect with us

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amechaguliwa bila kupingwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa baraza la vyama vya soka kwa nchi za Afrika Mashariki Cecafa.

Uchaguzi huo umefanyika leo jijini Nairobi, ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Senior Chalenji Cup.

Karia amekuwa rais wa TFF tangu Oktoba mwaka huu kwenye uchaguzi uliofanyika Mkoani Dodoma, katikati ya Tanzania.

Wengine waliochaguliwa ni Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia) na Petra Dorris Kenya.

Wajumbe hao ambao wataungana na Rais wa kamati hiyo Mutasim Gafar wa Sudan watakuwa na kibarua kuboresha utenda kazi wa baraza hilo kwa ajili ya kuimarisha soka ukanda huo.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in