Connect with us

Kenya imeshinda taji lake la saba kama bingwa wa mchezo wa soka kati ya mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA.

Harambee Stars, ilipata ubingwa wa mwaka 2017 Jumapili iliyopita, baada ya kuifunga Zanzibar kupitia mikwaju ya penalti.

Kenya iliondoka na ushindi wa mabao 3-2, baada ya mchuano huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos, baada ya muda wa kawaida na ule wa ziada.

Ushindi huu, umeirejesha Kenya katika ubingwa wa soka la ukanda, baada ya kuwa katika nafasi hiyo mara ya mwisho mwaka 2013.

Miaka mingine ambayo Kenya imeshinda taji hili ni mwaka 1975, 1981, 1982, 1983 na 2002.

Katika kipindi ambacho Harambee Stars imekuwa bingwa wa CECAFA, imeibuka mshindi mara tatu ikiwa mwenyeji mwaka 1983, 2013 na 2017.

Historia ya Kenya katika fainali ya CECAFA:-

1975- Kenya 5-4 Malawi

1981-Kenya 1-0 Tanzania

1982-Kenya 5-3 Uganda

1983-Kenya 1-0 Zimbabwe

2002-Kenya 3-2 Tanzania

2013-Kenya 2-0 Sudan

2017 Kenya 3-2 Zanzibar

Pamoja na mafanikio haya, Uganda inaendelea kushikilia rekodi ya kushinda mataji mengi katika michuano hii.

Uganda Cranes ambayo ilimaliza katika nafasi ya tatu katika mashindano ya mwaka 2017, mataji 14, mwisho ikiwa ni mwaka 2015.

Ethiopia inashikilia nafasi ya tatu kwa kushinda mataji manne, huku Tanzania nayo ikishinda mara tatu.

Zanzibar ambayo ilifika fainali mwaka 2017, imewahi kushinda taji hili mwaka 1995.

More in