Connect with us

Kenya na Ghana kumenyana uwanjani Ohene jijini Accra

Uwanja wa Ohene jijini Accra nchini Ghana

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza kuwa mechi ya mwisho kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwezi Juni nchini Misri, kati ya Black Stars ya Ghana na Harambee Stars ya Kenya, itachezwa katika uwanja wa Ohene jijini Accra.

Ghana ambao wameshinda taji la Afrika mara nne, walipoteza mechi ya kwanza, jijini Nairobi bao 1-0 mwezi Septemba mwaka 2018.

Black Stars, haijawahi kucheza katika uwanja wa Kimataifa wa Accra baada ya kuishinda Mauritania mabao 7-1 katika mechi ya kufuzu kucheza fainali za bara Afrika mwaka 2017.

Mechi hiyo itachezwa tarehe 23 mwezi huu. Timu zote mbili zimefuzu katika michuano hiyo ya AFCON 2019.

More in African Football