Connect with us

Kenya na Tanzania kuchuana katika mechi ya kirafiki

Kenya na Tanzania kuchuana katika mechi ya kirafiki

 

Timu ya Taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars itamenyana na Taifa Stars ya Tanzania katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki.

Mchuano huo utapigwa tarehe 29 mwezi Mei jijini Nairobi.

Kenya na Tanzania zitatumia mchuano huo kwa maandalizi ya mchuano wa kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika, itakayofanyika nchini Gabon mwaka ujao.

Harambee Stars inajiandaa kucheza na Congo Brazaville tarehe 3 mwezi Juni huku Tanzania ikimenyana na Misri tarehe 4 pia mwezi huo.

Kenya ambayo haiwezi kufuzu katika michuano hiyo, ni ya mwisho katika kundi E, kundi ambalo linaongozwa na Guinea Bissau ikifuatwa na Congo kisha Zambia.

Tanzania nayo haina nafasi ya kufuzu kwa sababu Chad ilijiondoa na kundi hilo la G kwa sababu za kifedha, linasalia na Misri ambao kimahesabu wamefuzu na Nigeria tayari wameondolewa.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya Nick Mwendwa amesema, Harambee Stars inataka kuanza kucheza mechi za Kimataifa za kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in