Connect with us

Timu ya soka ya Kenya All Stars inayowajumuisha wachezaji kutoka vlabu mbalimbali walifungwa na klabu ya Uhispania ya Cordoba mabao 4-0 katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa siku ya Jumatano usiku.

 

Mabao ya klabu ya Cordoba FC inayocheza ligi ya daraja la pili ilipata mabao yake kupitia Nathan Mejia, Jose Fernandez, Alberto Quiles na Alejandro Alfaro.

Mchuano huo ulichezwa katika uwanja wa Nuevo Arcangel mjini Cordoda.

Kocha wa Kenya All Stars Stanley Okumbi alifanya mabadiliko kadhaa katika kikosi chake lakini juhudi zake za kutafuta mabao hazikufua dafu.

Mchuano huo uliandaliwa na viongozi wa ligi kuu nchini Kenya na La Liga nchini Uhispania.

Klabu ya Cordoba inajiandaa kwa msimu mpya wa ligi mwezi Agosti huku Kenya ikitumia kikosi chake kitawakilisha nchi hiyo  wakati wa mashindano ya CHAN mwaka ujao.

Baada ya mechi hii, Kenya inatarajiwa kucheza mchuano mwingine wa kirafiki dhidi ya Sevilla Atlético siku ya Jumanne wiki ijayo.

Kikosi cha Kenya All Stars-

Makipa: Bonface Oluoch (Gor Mahia), Matthias Kigonya (Sofapaka).

Mabeki: Musa Mohammed (Gor Mahia), Robinson Kamura (AFC Leopards), Maurice Ojwang’ (Western Stima), Wesley Onguso (Sofapaka), Benson Iregi (Thika United) na Simon Mbugua (Posta Rangers).

Viungo wa Kati: Boniface Muchiri (Tusker), Clinton Kisiavuki (Nakumatt), Jackson Macharia (Tusker), Vincent Oburu (AFC Leopards) Victor Majid (AFC Leopards), Ovella Ochieng’ (Kariobangi Sharks) na Patillah Omoto (Kariobangi Sharks).

Washambuliaji: Samuel Onyango (Ulinzi Stars) na Victor Omondi (Nzoia Sugar).

More in