Connect with us

Kenya yaorodheswa ya 98 duniani huku Sudan na Ethiopia zikishuka

Kenya yaorodheswa ya 98 duniani huku Sudan na Ethiopia zikishuka

Kenya imeorodheshwa ya 98 duniani katika orodha ya hivi punde iliyotolewa na Shirikisho la soka duniani FIFA.

Orodha hii hutolewa kila mwezi na Harambee Stars imepanda nafasi 27 na kuingia katika orodha ya mataifa 100 bora duniani kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.

Mafanikio haya ya Kenya yanakuja baada ya kuishinda Cape Verde bao 1 kwa 0 na baadaye kufungwa mabao 2 kwa 0 katika michuano ya kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Uganda nayo imepanda nafasi 5 na sasa ni ya 62 baada ya ushindi mkubwa wa jumla ya mabao 4 kwa 0 katika michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia na tayari imefuzu katika hatua ya makundi baada ya kuishinda Togo nyumbani na ugenini.

Taifa Stars ya Tanzania nayo imepanda nafasi tatu na sasa ni ya 132 kutoka 135 mwezi uliopita.

Tanzania ilitoka sare ya mabao 2 kwa 2 nyumbani dhidi ya Algeria na baadaye kufungwa mabao 7 kwa 0 ugenini katika safari ya kucheza kombe la dunia.

Hata hivyo, Ethiopia imeendelea kufanya vibaya  baada ya kushuka nafasi sita na sasa ni ya 120 duniani sawa na Burundi ambayo ni ya 112.

Sudan ni ya 134 huku jirani yake Sudan Kusini ikiwa ya 138.

Ivory Coast inasalia timu bora barani Afrika na ya 19 duniani, Algeria ni ya pili na ya 28 duniani huku Ghana ikiwa ya tatu barani Afrika na ya 33 duniani.

Orodha nyingine kama hii itatolewa mwezi wa Januari mwaka 2016.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in