Connect with us

Mshambuliaji wa Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Shiza Kichuya amesema hana papara bali muda ukifika atakwenda kucheza soka nje ya Tanzania.

Mchezaji huyo mzaliwa wa Morogoro amekwa na wakati mzuri kwenye kikosi cha Simba tangu alipojiunga nayo mwaka 2016 akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Akizungumza na Mtandao huu kutoka Benin Kichuya amesema ni ndoto zake kucheza nje lakini hawezi kulazmisha kwa sababu kila mchezaji ana bahati yake.

“Mimi Kazi yangu ni kucheza soka, mengine nawaacgia wanaonisimamia. Nafurahia maisha Simba na ninaifurahia kazi yangu, kwa sasa nimewekeza nguvu kuhakikisha nashirikiana na wenzangu ili kuiwezesha Simba kushinda mataji mbalimbali,”alisema Mchezaji huyo ambaye pia amejihakikishia namba kwenye kikosi cha Kwanza cha Taifa Stars.

Kichuya ameifungia Simba mabao matano tangu ulipoanza msimu wa Ligi Kuu na anatajwa kama mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Simba

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in