Connect with us

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ipo jijini Monrovia nchini Liberia, kwa maandalizi ya mchuano muhimu kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano, kikosi hicho cha wachezaji 22 kimeanza kufanya mazoezi pamoja.

Hata hivyo, kikosi cha kocha Florent Ibenge kitawakosa wachezaji wanne ambao wana majeraha ambao ni Yannick YALA BOLASIA, Neeskens KEBANO, Arthur MASUAKU na Jordan IKOKO.

Kipa Ley MATAMPI MVUMI, hatakuwepo katika mchuano huo muhimu siku ya Jumapili kwa sababu klabu yake ya TP Mazembe haikumpa nafasi ya kuondoka kwa wakati na sasa nafasi yake imechukuliwa na Joel KIASSUMBUA.

  1. KIASSUMBUA Joël (Servette / Uswizi)
  2. MOSSI NGAWI Anthony (Chiasso FC / Uswizi)
  3. MABRUKI Nathan (DCMP / DR Congo)
  4. ISSAMA MPEKO Djos (TP Mazembe / DR Congo)
  5. DJUMA SHABANI Wadol (AS V.Club / RD Congo)
  6. Glody NGONDA ​​MUZINGA (AS V.Club / DR Congo)
  7. MOKE ABRO Wilfred (Koniaspor / Uturuki)
  8. LUYINDAMA NEKADIO Christian (Standard Liege / Ubelgiji)
  9. Yannick BANGALA LITOMBO (AS V.Club / DR Congo)
  10. MUNGANGA OMBA Nelson (AS V.Club / RD Congo)
  11. MAGHOMA Jacques (Birmingham City / Uingereza)
  12. MPOKU EBUNGE Paul-José (Standard Liege / Ubelgiji)
  13. NGOMA LUAMBA Fabrice (AS V.Club / RD Congo)
  14. MUBELE NDOMBE Firmin (Toulouse / Ufaransa)
  15. KABANANGA KALONJI Junior (Astana FC / Kazakhstan)
  16. MESCHAK ELIA Lina (TP Mazembe / DR Congo)
  17. BOLINGI MPANGI Jonathan (Antwerp /Ubelgiji)
  18. AFOBE TUNANI Benik (Stoke City / Uingereza)
  19. ASSOMBALANGA Britt (Middlesbrough FC / Uingereza)
  20. AKOLO Chadrack (Stuttgart / Ujerumani)
  21. UNGENDA MUSELENGE Bodrick (Primeiro d’Agosto / Angola)
  22. LEMA MABIDI Chikito (Raja Casablanca Club / Morocco)

More in