Connect with us

Na Fadhili Sizya

Kipa mkongwe Ivo Mapunda ametangaza kusaka klabu ya kucheza soka kutoka nje ya nchi baada ya kutumikia  kwa muda mrefu katika soka la Tanzania.

 

Akizungumza katika mahojiano maalum na soka25east.com,alisema kuwa tayari anao uzoefu mkubwa kucheza soka la nyumbani hivyo anafikiri nafasi kubwa ya kuendelea kufanya vizuri ataipata ikiwa atacheza soka la kulipwa.

 

Aidha kipa huyo alisema kwa sasa anacho kituo cha kulelea vijana wa soka (football academy) ambapo yupo katika mipango ya kukiimarisha huku akijipanga na yeye kuendelea binafsi.

 

Pia Mapunda alithibitisha kufuta uvumi wa kutangaza kustaafu na ukimya wake katika soka ni kujipanga katika soka la kulipwa.

 

Hata hivyo Mapunda aliwahi kucheza klabu za Yanga, Moro United, Simba Sc, African Lyon, Azam Fc na nje ya Tanzania aliwahi kucheza Gor Mahia, St George na kuwa kulitumia taifa la Tanzania akiwa kipa namba moja

 

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

More in