Connect with us

Nah Clarissee Uwimana,

Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Yannick Mukunzi anesajiliwa na klabu ya Rayon Sports kutoka APR pia ya Rwanda.

APR ilikuwa inasuasua kumsainisha mkataba mpya Mukunzi kabla ya Rayon kuingilia kati.

APR na Rayon zina upinzani mkubwa katika soka la Rwanda na kumekuwa na upinzani kwa mchezaji kuhama kutoka timu moja hadi nyingine.

Mukunzi amevuna Faranga milioni 10 na kuzikataa Faranga milioni 8 alizoahidiwa na APR ili asaini mkataba mpya.

Wachezaji wengine walioihama APR tangu msimu uliopita ni Abdul Rwatubaye, Rwigema Yves na Nova Bayama.

Rais wa Rayon Sports Gacinya Dennis alithibitishia ntandao wa soka25east kuwa klabu yake imemnasa Mukunzi.

More in