Connect with us

Kiungo wa Yanga, Juma Mahadhi amewaomba radhi mashabiki wasoka wa klabu hiyo kutokana na kuwa na kipindi kigumu kilichochangiwa na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha Yanga.

Mahadhi alisajiliwa na Yanga mwaka 2016 akitokea Coastal Union ya Tanga lakini tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara mchezaji huyo amekosa kabisa nafasi ya kucheza katika timu hiyo.

Mechi ya mwisho kwa Mahadhi kuonekana uwanjani ilikuwa baina ya Simba na Yanga, mchezo wa kuwania ngao ya hisani ambpao alipoteza mkwaju wa penati. Kukosa nafasi ya kucheza kumepelekea mchezaji hutyo kupoteza nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’

Mahadhi ametuymia ukurasa wake wa Instagram kuomba nafasi ya kuaminika na timu yake ikiwa bado inamhitaji.

“Nimejifunza mengi, naahidi kuwa Mahadhi mpya,naomba imani yenu kwangu kama bado mnaona ninahitajika katika timu yangu pendwa ya Yanga. Natumaini kilio changu kimewafikia nahitaji sasa kuanza mwaka mpya nikiwa kijana mwema na mpya,”aliandika mchezaji huyo aliyechipukia kisoka Mkoani Tanga.

Mahadhi anakumbukwa kwa kiwango bora alichokionyesha wakati Yanga ilipopambana na TP Mazembe katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Juni, 2016.

 

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in