Na Victor Abuso, Lushoises OCL City ndio mabingwa wa soka taji la wanawake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuwashinda Recoilless ya Mbuji-Mayi mabao 3 kwa 0 katika mechi ya fainali. Hili ni taji la nne mfululizo kwa klabu ya Lushoises, iliyoanza kushiriki soka la wanawake nchini humo tangu mwaka 2012. Mwaka uliopita, vlabu hivi vilikutana tena katika hatua ya fainali na akina dada kutoka Lubumbashi wakaendelea kudhihirisha kuwa wao ni moto wa kuotea mbali. Nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Bafana Bafana Katanga baada ya kuwafunga Mornng Star kutoka North Kivu mabao 6 kwa 1. Mikoa 9 kati ya 11 ilishiriki katika makala haya ya nane ya michuano hii huku mikoa ya Kasai Occidental na Ecuador ikijiondoa kwa sababu za changamoto za kifedha. Orodha ya vlabu vilivyoshiriki katika ligi hiyo:- Bilenge (Kinshasa) Bafana Bafana (Katanga) RC Boa (Maniema) Promo Sport (Bas-Congo) GTT (Bandundu) Attack recoilless (Kasai Oriental) Morning Star (South Kivu) OCL into City (Katanga) Orodha ya mabingwa wa taji hilo 2008 South Kivu 2009 Kinshasa 2010 Kinshasa 2011 Katanga 2012 OCL City 2013 OCL City 2014 OCL City 2015 OCL City.
Klabu ya wanawake ya Lushoises OCL City mabingwa nchini DRC
Klabu ya wanawake ya Lushoises OCL City mabingwa nchini DRC
More in
-
Nigeria Super Falcons break jinx and qualify for Paris 2024 Olympics
Nigeria Super Falcons have qualified for the 2024 Paris Olympic Games. Nigeria beat South...
-
Zambia Copper Queens qualify for 2024 Paris Olympics
The Zambia Women’s National Team, The Copper Queens have booked a place at the...
-
Cameroon sports Minister appoints Indomiable lions coach in Bizzare move
Cameroon Sports minister Narcisse Mouelle Kombi has appointed Belgian Marc Brys as the new...
-
Simba lose to Al Ahly at home in first leg Quarter-final
Tanzanian giants Simba SC suffered a devastating 1-0 defeat to record holders Al Ahly...