Connect with us

Ufaransa inatarajiwa kuwatumia wachezaji wake wenye uwezo mkubwa Kylian Mbappe na Antoine Griezmann kujaribu kuwazuia Ubelgiji, kupata ushindi muhimu wakiongozwa na Eden Hazard, katika mchuano wa kihistoria wa nusu fainali, kuingia fainali ,  kuwania kombe la dunia, mchezo utakaopigwa siku ya Jumanne usiku mjini Saint Petersburg nchini Urusi.

Ufaransa inatarajiwa kufika katika hatua ya fainali, kwa mara ya kwanza, mwisho ikiwa ni mwaka 2006, walipofungwa na Italia, lakini Ubelgiji nayo ina imani kuwa, itaweka historia kwa kufuzu katika hatua ya fainali kwa mara ya kwanza.

Ubelgiji inakwenda katika mchuano huu, ikiwa na historia pekee ya kucheza katika hatua ya nusu fainali mwaka 1986 ilipofungwa na Argentina mabao 2-0.

Kufika katika hatua hii,Ufaransa walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uruguay huku Ubelgiji wakiishinda Brazil mabao 2-1.

Mshindi katika mechi hii atamenyana na Croatia au Uingereza, katika fainali itakayochezwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Luzhniki .

Ratiba ya Jumatano:-

Croatia vs Uingereza-Uwanja wa Luzhniki jijini Moscow

 

More in FIFA World Cup