Connect with us

Michuano ya kombe la dunia inaanza siku ya Alhamisi kati ya wenyeji Urusi na Saudi Arabia.

Mechi hii itachezwa katika uwanja wa Luzhniki jijini Moscow kuanzia saa 12 jioni saa za Afrika Mashariki.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amekuwa akisema kuwa nchi yake iko tayari kwa michuano hiyo na amewakaribisha mashabiki wa soka kote duniani katika nchi yake.

Mataifa 32 akiwemo bingwa mtetezi Ujerumani anashiriki katika michuano ya mwaka huu.

Kutakuwa na michuano 64 zitakazochezwa kwa siku 32 zijazo.

Fainali hii ya 21 ya kombe la dunia, itachezwa katka viwanja 12 katika miji 11 nchini humo.

Panama na Iceland yanashiriki katika mashindano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Afrika inawakilishwa na mataifa matano ambayo ni pamoja na Misri, Senegal,Tunisia, Nigeria na Morocco.

Ratiba ya Jumanne, Juni 15 2018

Misri vs Uruguay-Mjini Ekaterinburg

Morocco vs Iran-Mjini St.Petersburg

Ureno vs Uhispania-Mjini Sochi

More in African Football