Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Mashabiki wa soka nchini wanalazimika kuanza kujikamua mapema ili washuhudie mchezo wa Ligi Kuu baina ya wapinzani wa jadi Simba na Yanga.

Timu hizo zitavaana Jumamosi Oktoba 28 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa mzunguko wa nane.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Alfred Lucas amesema kiibgilio cha chini cha mchezo huo ni shilingi 10,000 za Tanzania sawa na dola nne na nusu.

“Jukwaa kuu ni shilingi 20,000 na mzunguko ni 10,000. Nawasihi mashabiki wanunue mapema tiketi za mchezo hup ili kuepuka usumbufu,”amesema Lucas.

Mechi hiyo imeshaanza kuwa gumzo jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla huku washambuliaji Emanuel Okwi na Ibrahim Ajibu wakitajwa sana na mashabiki wa soka.

Okwi anayeichezea Simba amefunga mabao nane katuka ligi kuu akifuatiwa na Ajibu wa Yanga ambaye amefunga mabao matano.

More in