Connect with us

Wafaransa wanaendelea kusherehekea kombe la dunia, baada ya kuishinda Croatia mabao 4-2 katika fainali iliyochezwa nchini Urusi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mbali na sherehe hizo, kuna swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwanini mara zote, idadi kubwa ya wachezaji ni weusi ?

Kabla ya kujibu swali hili, hiki ndicho kikosi kamili cha timu hii ya taifa:-

Makipa: Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Marseille), Alphonse Areola (Paris Saint-Germain).

Mabeki: Djibril Sidibe (Monaco), Benjamin Pavard (Stuttgart), Samuel Umtiti (Barcelona), Raphael Varane (Real Madrid), Presnel Kimpembe (Paris Saint-Germain), Adil Rami (Marseille), Benjamin Mendy (Manchester City), Lucas Hernandez (Atletico Madrid).

Viungo wa Kati: Paul Pogba (Manchester United), Corentin Tolisso (Bayern Munich), Blaise Matuidi (Juventus), Ngolo Kante (Chelsea), Steven Nzonzi (Sevilla).

Washambuliaji: Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Olivier Giroud (Chelsea), Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain), Ousmane Dembele (Barcelona), Florian Thauvin (Marseille), Nabil Fekir (Lyon), Thomas Lemar (Monaco

Mbali na kikosi hiki cha sasa, kilichoshinda kombe la dunia, wachezaji wengine maarufu weusi waliowahi kuwa katIka timu ya taifa ni pamoja na Nicolas Anelka, Thierry Henry, Lilian Thuram, Patrick Vierra, Eric Abidal bila kumsahau Zinadene Zidane miongoni mwa wengine wengi.

Sababu kubwa ya suala hii ni kwa sababu ya sheria ya Ufaransa ambayo hairuhusu kuhesabiwa na watu waliongia nchini humo, ili kuepuka ubaguzi.

Waafrika wengi hasa kutoka Afrika Magahribi waliingia nchini Ufaransa miaka ya zamani kabla ya mapinduzi na kuwa raia wa nchi yao na hivyo, watoto wao ni Wafaransa.

Hii ni sera ambayo imewapa nafasi, wachezaji wenye rangi mbalimbali kujitokeza na kushiriki katika michezo hasa soka, kutokana na Ufaransa kuwa na watu kutoka mabara yote.

Wachambuzi wa soka wanaona kuwa, mafanikio ya Ufaransa yametokana na mchanganyiko wa watu Weusi, Wazungu na Waarabu katika kikosi hicho.

Licha ya Ufaransa kuendelea kukabiliwa na changamoto za wahamiaji haramu hasa Waafrika, miaka ya hivi karibuni, imeanza kutoa nafasi kwa mhamiaji anayeonekana kuwa na uwezo wa kuisaidia nchi hiyo kama raia wa Mali, Mamoudou Gassama aliyemwokoa mtoto juu ya jengo la Orofa na kupewa uraia.

Jambo lingine ni uhusiano mwema kati ya kocha wa sasa, Didier Dechamps ambaye ameonekana kuwakumbatia wachezaji wote hasa weusi.

Mwaka 2010, Ufaransa ilishindwa katika hatua ya makundi baada ya kile kinachoelezwa kuwa uhusiano mbaya kati ya kocha wa wakati huo Raymond Domenech na wachezaji weusi hasa Patrice Evra.

Mwaka 1998, Ufaransa iliposhinda kombe hili kwa mara ya kwanza baada ya wachezaji weusi waliokuwepo katika kikosi hicho ni pamoja na, Patrick Vieira, Marcel Desailly, Thierry Henry, Bernard Diomende na Lilian Thuram walioongeza nguvu na Le Blues kuishinda Brazil mabao 3-0.

Kocha wa wakati huo alikuwa ni Mfaransa Aimé Jacquet.

 

More in