Connect with us

Le Roy akitaja kikosi cha kuvaana na Zambia

Le Roy akitaja kikosi cha kuvaana na Zambia

 

Kocha wa timu ya taifa ya Togo Claude Le Roy amekitaja kikosi cha wachezaji 21 kucheza na Zambia katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki wiki ijayo.

Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na mchezaji wa Kimataifa wa klabu ya Crystal Palace Emmanuel Adebayor.

Mchuano huo utapigwa mjini Lome lakini mchuano huo pia utatumiwa kujiweka tayari kupambana na Liberia katika mchuano muhimu wa kufuzu kucheza fainali ya Afrika mwaka ujao nchini Gabon.

KIKOSI KAMILI:

Makipa: Cedric Mensah (Colma),Baba Tohagouni (Marmand),Kossi Agassa (Reims).

Mabeki: Serge Akapo (Trabzonspor),Gafar Mamah (Dacia),Kakou Donu (Rangers Int’l),Joseph Douhadji (Rivers),Sadat Akonko (Al Faysaly),Djenne Dakonam (Alcorcon).

Viungo wa Kati: Prince Segbefia (Unattached),Alaixys Romao (OM),Henrise Eniful (Doxa),Dove Wome (Supersport),Kossivi Nouwokio (Asec Mimosas),Floyd Ayite (Bastia),Lalawele Atakwa (Helsingborgs),Mathieu Dossevi (Standard Liege).

Washambuliaji: Emmanuel Adebayor (Crystal Palace),Camaldine Abraw (Kaizer Chiefs),Jonathan Ayite (Alanyspor),Robert Dussey (Atalanta Bergama).

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in