Connect with us

Kocha mpya wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre amesema kazi inayomkabili ni kuhakikisha Simba inaimarika zaidi na kuwa na uwezo wa kutwaa mataji katika michuano mbalimbali.

Kocha huyo jana aliingia kandarasi ya kuifundisha Simba ambayo haikuwekwa wazi lakini duru zinasema ameingia mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam baada ya kutambulishwa rasmi kocha huyo amesema Simba ina wachezaji wazuri na kinachotakiwa ni kufanya kazi kila mmoja.

“Nimeiangalia Simba ina wachezaji wazuri sana tunachotakiwa ni kuimarika zaidi. Sipendi kuzungumza mengi, nimekuja kufanya kazi,”alisema Kocha huyo ambaye mwaka 2000 aliiongoza Camerron kutwaa taji la mataifa ya Afrika.

Lechantre ataanza kazi Jumanne ijayo.

Simba iko Mjini Bukoba, Mkoani Kagera ambako Jumatatu itachuana na Kagera Sugar katika mechi ya Ligi Kuu inayotabiriwa kuwa itakuwa na upinzani mkubwa.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in