Connect with us

 

Kundi la kwanza la wachezaji 16 wa timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Leopard, wamekwenda nchini Namibia kushiriki katika michuano ya kusaka ubingwa wa taji la Kusini mwa Afrika COSAFA iliyoanza wiki hii.

Michuano hii inafanyika nchini Nambia na DRC itaanza kushiriki michuano hii katika hatua ya robo fainali dhidi ya Msumbiji.

Mongoni mwa wachezaji watatu wa kulipwa wanaoshiriki katika kikosi hiki ni pamoja na Hervé Lomboto anayechezea klabu ya Leopards Dolisie ya Congo Brazzaville, Bobo Ungenda kutoka Kabuscorp ya Angola na André Bukia anayechezea klabu ya Boa Vista ya Ureno.

Mechi za robo fainali itaanza siku ya Jumamosi, baada ya kumalizika kwa mechi za makundi.

Ratiba Jumamosi Juni 18 2016

Afrika Kusini vs Mshindi wa Kundi la B

Namibia vs Bostwana

Jumapili Juni 19 2016

Zambia vs Mshindi wa Kundi la A

DR Congo vs Msumbuji

Fainali itachezwa tarehe 24 mwezi huu jijini Windhoek.

More in