Connect with us

 

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, ametoa kitita cha Dola za Marekani 200,000 kama zawadi kwa timu ya taifa ya soka ya Leopard ambayo imefuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika itakayofanyika mwaka ujao nchini Gabon.

Kocha Florent Ibenge aliiongoza Leopard kufuzu katika fainali yake ya 16 ya AFCON baada ya kuifunga Jamhuri ya Afrika ya Kati mabao 4-1 katika uwanja wa Tata Rafael jijini Kinshasa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Tuzo hii imekuja baada ya rais Kabila kuwatuza wachezaji wanaocheza soka nyumbani magari ya kifahari baada ya kushinda ubingwa wa CHAN wa bara la Afrika, fainali iliyofanyika mwezi Januari nchini Rwanda.

DRC ilishiriki mara ya kwanza katika michuano hii mwaka 1965 na imeshinda taji hili mara mbili mwaka 1968 na 1974.

More in Africa Cup of Nations