Connect with us

Michuano ya kwanza ya kutamatisha makundi katika makala ya tano ya michuano ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani barani Afrika, inachezwa Jumanne usiku.

Itakuwa ni zamu ya kundi D, ambalo limekutanisha timu za Angola, Cameroon, Congo na Burkina Faso.

Mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Angola na Burkina Faso, mechi itakayochezwa katika uwanja wa Adrar mjini Agadir kuanzia saa moja na nusu, saa za Afrika Mashariki.

Kabla ya michuano hii, Angola wameshiriki mara tatu katika michuano hii, huku Burkina Faso wakicheza mara mbili, mwisho ikiwa ni mwaka 2014.

Cameroon ambao mwaka 2011 na 2016, walifika katika hatua ya robo fainali ya michuano hii, itafungua mechi yake ya kwanza dhidi ya Congo Brazaville ambayo inacheza katika michuano hii kwa mwaka wa tatu.

Siku ya Jumatatu, mabingwa mwaka 2014 Libya, walianza vema baada ya kuifunga Equatorial Guinea kwa mabao 3-0.

Saleh Al Taher aliifungia timu yake mabao mawili, dakika 12 na 17 kipindi cha kwanza huku Zakaria Al Harash, akimaliza kazi kwa kufunga bao la tatu katika dakika ya 86 ya mchuano huo.

Nigeria nayo ilipata wakati mgumu mbele ya Rwanda katika uwanja wa Ibn Batouta, mjini Tangier baada ya kutofungana 0-0.

Libya inaongoza kundi la C kwa alama 3, huku Nigeria na Rwanda ikiwa na alama 1.

 

Ratiba ijayo: Kundi A Januari 17 2018

Morocco v Guinea

Sudan v Mauritania

Januari 18 2018-Kundi B

Ivory Coast v Zambia

Uganda v Namibia

Januari 19 2018-Kundi C

Libya v Nigeria

Rwanda v Equitorial Guinea

 

More in