Connect with us

Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea tena baada ya mapumziko ya majuma mawili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Leo Jumapili, Tanzania Prisons inaialika Mbeya City katika mchezo unaotabiriwa kuwa na ushindani mkali kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizo mbili. Mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa sokoine Jijini Mbeya.

Kesho Jumatatu, Njombe Mji itakuwa na kibarua kizito itakapoialika Kagera Sugar, mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe.

Siku ya Jumatano ya Julai 17, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Yanga watakuwa wenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Yanga itatakiwa kushinda mchezo huo ili kuendelea kuifukuza Simba ambayo inaizidi kwa alama tano.

Alhamisi, Julai 18, Simba ambayo iliwachukiza mashabiki wake baada ya kufanya vibaya kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi itaialika Singida United, mchezo unaotabiriwa utakuwa na upinzani kutokana na timu hizo kuwa na wachezaji imara.

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in