Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18 inaanza leo kwa michezo itakayopigwa katika viwanja mbalimbali.

Makamu bingwa wa msimu uliopita Simba itakuwa mwenyeji wa Wanajeshi Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa huku Mbao FC ya Mwanza itakuwa ugenini mjini Bukoba kupamban na Kagera Sugar.

Mtibwa Sugar itaialika Stand United mkoani Morogoro wakati Mwadui FC itacheza na Singida United iliyopanda daraja.

Mkoani Mtwara Azam itapambana na Ndanda na Mjini Njombe timu iliyopanda daraja ya Njombe Mji itaipokea Tanzania Prisons.

Mbeya City itakuwa kwenye uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya kucheza na Majimaji ya Songea.

Mabingwa watetezi wa Ligi, Yanga yenyewe itashuka uwanjani Jumapili kucheza na Lipuli ya Iringa ambayo imepanda daraja msimu huu.

Ligi ya msimu huu inatabiriwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na usajili uliifanywa na timu shiriki.

More in African Football