Connect with us

Luka Modric, kiungo wa kati wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Croatia, ndio mshindi wa tuzo ya mwaka 2018 ya Ballon d’Or .

Modric, mwenye umri wa miaka 33, amevunja rekodi ya zaidi ya miaka 10, ambayo imekuwa ikitawaliwa na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Mchezaji huyo, amepata tuzo hiyo, baada ya kuisadia klabu yake, kunyakua ligi kuu ya soka nchini Uhispania mara tatu mfululizo.

Aidha, alikuwa wa msaada mkubwa, alipoisadia timu yake ya taifa kufika fainali ya kombe la dunia, licha ya kufungwa na Ufaransa mabao 4-2 mwezi Julai huko nchini Urusi.

Najiskia vema sana. Nimefurahi na nanyenyekea sana. Nina hisia nyingi sana wakati huu, sina maneno ya kusema,” alisema Modric baada ya kutajwa mshindi, Jumatatu usiku.

Tuzo la Ballon d’Or ilianza kutolewa mwaka 1956, lakini ilianza kushirikiana na FIFA kati ya mwaka 2010 hadi 2015.

Waandaji wa tuzo hii ni Gazeti la Ufaransa la soka la, France Football.

Cristiano Ronaldo ameshinda taji hili mara tano, mwaka 2008, 2013, 2014, 2016 na 2017 huku Lionel Messi pia akishinda mara tano mwaka 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015.

More in Swahili Stories