Connect with us

African Football

Lweza FC yalazimisha sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya URA

Lweza FC yalazimisha sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya URA

Klabu ya soka ya KCCA nchini Uganda, inaendelea kuongoza ligi kuu ya soka nchini humo kwa alama 29 baada ya kupata ushindi muhimu wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Soana FC, siku ya Jumanne jioni katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala.

Mabao ya KCCA yalitiwa kimyani na Samson Ceasar Okhuti, mabao ya kwanza kuifungia klabu yake kwa mara ya kwanza tangu mwezi Januari.

Express F.C ilifungwa na JMC mabao 2 kwa 0 mjini Jinja, katika uwanja wa Kakindu.

Mabao ya Express FC nayo yalifungwa na nahodha Richard Wandyaka na Musa Walangilira katika mchuano huo.

Katika uwanja wa Mutesa II, Wankulukuku jijini Kampala klabu ya URA FC ilitoka sare ya bao 1 kwa 1 na Lweza FC.

Lweza FC ilionekana kufanya vizuri katika mchuano huo lakini ilishindwa kuzuia URA kufunga na sasa ni ya 12 kwa alama 16 baada ya kucheza michuano 15.

Matokeo kamili:-

KCCA F.C 2-0 Soana F.C

JMC Hippos F.C 2-0 Express F.C

Lweza F.C 1-1 URA F.C

Bright Stars F.C 0-0 BUL F.C

The Saints  F.C 0-1 Sadolin Paints F.C

Maroons 0-1 SC  Victoria University

More in African Football