Connect with us

Maandalizi ya AFCON yanaendelea vizuri

Siku 100 kuelekea fainali ya kuwania ubingwa wa taji la soka baina ya mataifa ya Afrika nchini Misri, kamati andalizi inasema maandalizi yanakwenda vizuri.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hany Abo Rida, ameiambia tovuti ya Shirikisho la soka barani Afrika, cafonline.com kuwa, michuano hiyo itasalia katika kumbukumbu ya mashabiki wengi wa soka wakati na baada ya kumalizika.

Misri itakuwa nchi ya kwanza, kuandaa fainali hii ambayo kwa mara ya kwanza itakuwa na mataifa 24 katika michuano itakayofanyika kati ya tarehe 21 hadi Julai mwaka 2019.

Tayari Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza kuwa droo ya fainali hiyo itafanyika tarehe 12 mwezi Aprili.

Baadaye mwezi huu, michuano ya mwisho kufuzu katika fainali hii, itachezwa katika viwanja mbalimbali.

Miongoni mwa mataifa ambayo hadi sasa yamefuzu katika michuano hii ni pamoja na wenyeji Misri, Madagascar, Senegal, Morocco, Mali, Algeria, Nigeria, Kenya, Ghana, Guinea, Ivory Coast na Mauritania.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in